Asubuhi njema wanamafanikio?
Hongera sana kwa siku hii nyingine ya leo,
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo makubwa.
Tutumie nafasi hii ya leo vizuri rafiki yangu.

img_20161112_091656

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MSINGI…
Popote ambapo unaona mambo hayaendi sawa, tatizo linaanzia kwenye msingi.
Kama ilivyo kwenye nyumba, msingi ndiyo unabeba uimara wa nyumba. Kama nyumba imejengwa kwenye msingi usio imara, nyumba hiyo haitakuwa imara.
Kama nyumba imejengwa kwenye msingi imara, itakuwa imara na kudumu kwa muda mrefu.
Sasa, kila kitu tunachofanya kwenye maisha yetu, kuna msingi ambao tunaanza nao.
Iwe ni mahusiano, kazi, biashara na kingine chochote, kuna msingi ambao tunaanza nao.
Msingi huu ndiyo unaamua ikiwa tunachofanya kitadumu muda mrefu na kufanikiwa au la.
Kama unajenga mahusiano yako kwenye msingi wa uaminifu na kuheshimiana, basi mahusiano hayo yatadumu.
Kama unajenga biashara yako kwenye misingi ya kazi, uadilifu, kujituma, nidhamu na kujifunza zaidi, biashara yako inadumu.
Msingi una mchango mkubwa sana.
Anza na msingi sahihi na imara na utafika popote unapotaka kufika.

Nakutakia siku njema sana.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info