Habari za leo rafiki?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tulichochagua kufanya.

img_20161112_091656
Rafiki, muda wa leo ukipita, hautorudi tena, hivyo utumie vizuri.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUWEZA vs KUFANYA…
Kuna watu ambao wanakaa chini na kufanya kitu, kitu kikubwa na cha kipekee. Halafu wakishafanya, wanakuja wengine na kusema hata wao wanaweza kufanya, tena wangefanya kwa ubora zaidi.
Jambo la kushangaza ni kwamba kwa nini hawa wanaodai wanaweza hawakufanya? Kwa nini wasubiri mpaka mtu afanye ndiyo waje na habari zao kwamba wanaweza vizuri zaidi?

Jibu ni kwamba wanaofanya ni WASHINDI na wanaosema wanaweza kufanya ni washindwa.
Hivyo wewe rafiki yangu, chagua kukaa upande wa washindi.
Usiwe mtu wa maneno mengi, bali kuwa mtu wa vitendo.
Kama kuna kitu unaweza kufanya vizuri, kaa kimya na fanya.
Matendo yanaonekana kuliko maneno.
Waache washindwa wapige maneno, wewe kuwa mtu wa vitendo.
Tuonyeshe unachofanya, usituambia unachoweza kufanya.
Kuweza kufanya na kufanya ni vitu viwili tofauti.
Unahitaji nidhamu kuweza kukaa chini na kufanya.
Washindwa hawana nidhamu hii.

Leo nenda kafanye kitu rafiki, fanya kitu kitakachokusogeza mbele kufikia mafanikio yako.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info