Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho tumechagua kufanya.

img-20161217-wa0002
Muda uliopata leo huwezi kuupata tena, hivyo utumie vizuri sana.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MATOKEO.
Kile ambacho tunakiona kwenye maisha yetu ni matokeo ya vitu ambavyo tumefanya au kutokufanya huko nyuma.
Na hii ina maana kwamba tatizo siyo kile tunachokiona kwenye maisha yetu (matokeo), bali tatizo ni yale mambo ambayo tumefanya au kutofanya na kupelekea kupata matokeo ambayo tumepata sasa.
Hivyo kama tunataka kubadili au kuboresha maisha yetu, hatuwezi kufanikiwa kama tutaangalia matokeo, tunahitaji kurudi kwenye mizizi na kuona nini tumefanya au hatukifanya na hivyo kupelekea kufika hapa tulipo sasa.

Biashara haiendi vizuri, angalia nini unafanya au hufanyi na hivyo kupelekea biashara kutokwenda vizuri.
Mambo yako hayajakaa sawa, angalia kuna namna umefanya au kutokufanya na ukapelekea mambo yako kutokukaa sawa.
Usikimbilie kubadili matokeo, kaa na angalia matokeo hayo yameletwa na nini. Na hapo ndipo unapoweza kufanya mabadiliko halisi.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info