Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Leo tumepata nafasi ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa zaidi ili tuweze kupata matokeo bora zaidi.

Muda wa leo ni kitu adimu sana, ukishapita hatuwezi kuupata tena. Tutumie kuda huu vizuri rafiki.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUHUDUMIA (SERVE).
Kama una wasiwasi ya kwamba kesho utapata wapi hela ya kula,
Kama una wasiwasi kama kweli utafikia mafanikio unayotaka,
Kama una wasiwasi ikiwa unachofanya kitakufikisha kwenye mafanikio,
Kumbuka jambo moja wakati wowote, SERVE, toa HUDUMA bora kabisa kwa wengine.
Hii ndiyo nguzo na ndiyo msingi pekee utakaokufikisha popote unapotaka.
Watu wana shida,
Watu wana maumivu,
Watu wana mahitaji,
Watu wana changamoto.
Wewe chagua ni eneo gani ambalo upo tayari kuwahudumia watu,
Eneo gani ambalo upo tayari kuweka juhudi na maarifa kuhakikisha maisha ya wengine yanakuwa bora zaidi.
Ni eneo gani ambalo unajua unaweza kuongeza thamani zaidi kwa wengine.
Jua eneo hili na lifanyie kazi.
Chochote unachotaka kwenye maisha yako, utakipata ikiwa utawasaidia watu wengi zaidi kupata kile ambacho nao wanataka.
Chochote unachotaka, utakipata kama utakuwa wa msaada kwa wengine.
Na iwapo utawahudumia wengine vizuri, hakuna siku hata moja ambapo maisha yatakuwa magumu kwako.
Unapoianza siku kila siku, swali la kukuongoza liwe ni huduma gani unakwenda kutoa kwa wengine, ni thamani gani unaongeza kwenye maisha ya wengine.
Popote ulipo, na chochote unachofanya, mwongozo wako uwe ni huu, WAHUDUMIE WENGINE, KUWA WA MSAADA KWA WENGINE, ONGEZA THAMANI KWA WENGINE na YAFANYE MAISHA YA WENGINE KUWA BORA ZAIDI.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info