Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Ni imani yangu kwamba umeianza siku ya leo vizuri sana na tayari una hamasa kubwa ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora. Hongera sana kwa hilo rafiki.

img-20161217-wa0002

Karibu tena kwenye tafakari zetu za kila siku. Kwa siku 10 zilizopita hatukuwa na tafakari kwa sababu tulikuwa na mafunzonya semina ya MWAKA 2017, MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO, ambayo yalifanyika kwa njia ya mtandao wa wasap kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA. Tumejifunza mengi na makubwa ya kuchukulia hatua mwakanhuu 2017 na kuendelea.

Asubuhi ya leo tutafakari kidogo zaidi kuhusu 2017…
Sasa tunamaliza wiki ya pili kwenye mwaka huu 2017,
Swali ni je, bado una ile hamasa uliyokuwa nayo siku ya kwanza na ya pili ya mwaka huu?
Je tayari umeshaanza kufanyia kazi yale ambayo umepanga kufanya mwaka huu?

Nakuuliza haya na wewe mwenyewe uyatafakari kwa sababu watu wamekuwa wakipata hamasa kubwa siku ya kwanza ya mwaka, na kuona kama mwaka utabadili kila kitu. Lakini siku chache baadaye wanarudi kwenye maisha yao ya kawaida na kuendelea vile vile.

Sitaki hili kitokee kwako rafiki yangu, ndiyo maana natakanutafakari yale uliyopanga kwa mwaka huu na kama upo kwenye uelekeo sahihi.
Jiulize hapo ulipo na kwa namna unavyofanya je utafika kule unakotaka kufika?
Kama jibu ni ndiyo, basi endelea kukaza mwendo, weka juhudi zaidi.
Kama jibu ni hapana, basi fanya mabadiliko sahihi yatakayokufikisha kule u akotaka kufika.
Usiendelee kujidanganya kwamba mabadiliko yatakufuata hapo ulipo, jua ya kwamba wewe ndiye wa kusababisha mabadiliko.
Na leo hii, NAMAANISHA LEO nenda kasababishe mabadiliko.

Nikutakie siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki yako
#KochaMakirita