Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwends kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora kabisa.

Tumia muda wa leo vizuri rafiki yangu.
Asubuhi ya leo tutafakari jinsi ambavyo tumekuwa tunakwepa kuchukua hatua.
Kuna mambo ambayo tumekuwa tunataka kufanya, lakini hatuanzi kufanya kwa kujiambia kwamba kwa sasa hatuna muda.
Na hivyo tunajiahidi ya kwamba tukipata muda tutafanya.
Rafiki, ukweli ni kwamba, hakuna mtu anayeweza kupata muda. Muda wetu kila siku ni ule ule, masaa 24 kwa siku.
Hivyo kama kuna kitu chochote tunataka kufanya, hatusubiri tupate muda, bali tunatenga muda na kukifanya.
Tatizo la kujiambia nikipata muda nitafanya ni kwamba huji kupata muda na hivyo kutokufanya.
Hivyo rafiki yangu, unapofikiria kufanya kitu, jiulize kama ni muhimu kwako.
Kama ni muhimu tenga muda wa kukifanya na kifanye, kama siyo muhimu achana nacho.
Lakini uaijidanganye kwamba utapata muda wa kufanya.
Muda haupatwi, muda unatengwa.
Tenga muda wa kufanya yale muhimu kwako rafiki.
Nikutakie siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Mimi rafiki yako,
#KochaMakirita