Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii bora na ya kipekee sana ya leo.
Ni nafasi nzuri kwetu ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.

Muda tulionao leo ni wa thamani sana, na hatuwezi kuupata tena baada ya muda huu kupita. Tutumie muda wetu wa leo vizuri sana.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kuchukua majukumu na kusubiri kupewa majukumu.
Hii ndiyo tofauti kubwa sana ya wale wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Wanaofanikiwa mara zote huwa wanachukua majukumu, huwa wanakuwa mstari wa mbele katika kufanya mambo na wanayafanya kwa kiwango kikubwa.
Ila wale ambao hawafanikiwi huwa wanasubiri mpaka wapewe majukumi. Hawawezi kuamua wao kama wao kuchukua majukumu, na hata yale majukumu wanayopewa, bado hawawezi kuyafanya kwa kiwango cha hali ya juu.
Asubuhi ya leo hebu tafakari wewe umekuwa upande gani? Umekuwa upande wa kichukua majukumu wewe mwenyewe, au umekuwa upande wa kusubiri mpaka upewe majukumu?
Tafakati na upate majibu yako, kisha chukua hatua.
Na hatua ya kuchukua leo ni kujipa jukumu ambalo utalifanya vizuri kabisa, utaweka juhudi kubwa na kuhakikisha unapata matokeo makubwa.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki yako,
#KochaMakirita