Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu, ambapo tuna jukumu kubwa la kwenda kuweka juhudi kubwa, kwa KUTHUBUTU, USHINDI NA SHUKRANI.

IMG_20170102_073855IMG_20170102_073855

Asubuhi ya leo tutafakari maisha kama mchezo,
Na kama ambavyo tunajua, kwenye kila mchezo kuna watu wa aina mbili,
1. Kuna wachezaji ambao wanakuwa ndani ya uwanja, wakipambana kupata ushindi.
2. Kuna washabiki ambao wapo nje ya uwanja, wakishangilia na kupiga kelele kulingana na wachezaji wanavyofanya.

Kwenye kila mchezo, shabiki ni rahisi sana kuona makosa ya wachezaji, na kila shabiki anajua kabisa ni njia ipi bora zaidi mchezaji angetumia. Utasikia shabiki anasema pale angepiga hivi, angeshinda goli.
Lakini tunajua ni rahisi kusema kuliko kufanya,
Ni rahisi kusema pale angefanya hivi kuliko kufanya mwenyewe.
Na hata wasiojua kabisa, na wao wanaweza kusema pale angefanya hivi.

Hivyo rafiki, asubuhi ya leo ondoka na haya mawili;
1. Usiwe shabiki, bali kuwa mchezaji. Usiseme pale angefanya hivi bali fanya kabisa. Usiwe mtu wa maneno, kuwa mtu wa vitendo. Fanya kitu leo.
2. Usiwasikilize sana mashabiki, wengi wanaongea tu kwa hisia, hawana utaalamu wowote ila ni rahisi kwao kusema pale angefanya hivi. Fanya lile unalojua ni sahihi, ka,a ukikosea basi jifunze. Unaposikia ushauri kutoka kwa mtu, jiulize naye ni mchezaji wa mchezo wowote au ni shabiki tu.

Fanya kitu leo rafiki yangu,
Nakutakia siku njema sana ya leo.
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
Kuwa na NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Makirita Amani,
#KochaMakirita