Habari za asubuhi rafiki yangu?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.

IMG_20170102_073855
Leo hii tunakwenda KUTHUBUTU, KUSHINDA NA KUSHUKURU.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu matokeo bora.
Kila mtu anapenda matokeo bora,
Kila mtu anapenda kuona matokeo makubwa,
Lakini matokeo haya hayaji tu yenyewe, bali ni zao la juhudi kubwa na mtazamo chanya pia.
Watu wengi wamekuwa wanawaangalia wale wanaopata matokeo bora na kuona hata wao wanataka matokeo yale.
Lakini wanasahau zile juhudi kubwa ambazo zimeleta matokeo yale.

Asubuhi ya leo tujikumbushe hili rafiki, matokeo bora yanazalishwa na juhudi kubwa, yanatokana na kujitoa kwa hali ya juu.
Hivyo mara zote jiandae kwa kwa hayo ili uweze kupata matokeo bora.

Nakutakia siku njema sana ya keo.
Rafiki yako,
#KochaMakirita