bari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Ni imani yangu kwamba umeianza siku ya leo kwa hamasa kubwa.
Tayari unajua nini unataka kwenye siku yako ya leo na umeshajipanga kupata kile unachotaka.

Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA utaweza kufanya mambo makubwa siku ya leo.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu WHATEVER IT TAKES,
Kupanga ni rahisi, tena sana. Unakaa chini na kufikiria nini unataka kisha kusema nataka hichi au kile.
Changamoto ipo kwenye utekelezaji wa mipango yako.
Pale unapoanza kutekeleza mipango yako, zinaibuka changamoto, vinatokea vikwazo vingi mno.
Unajikuta kuna vitu huna ili kukamilisha kile unataka,
Unashangaa watu ambao ulitegemea wakuunge mkono wanakuwa wa kwanza kukupinga.
Mambo yanakuwa magumu kiasi cha kufikia kukata tamaa.
Na hapa ndipo safari ya wengi inapioishia, na ndiyo maana wengi hawafanikiwi, wengi wanabaki na maisha ya kawaida.
Sisi wanamafanikio tunahitaji kula kiapo na nafsi zetu, ya kwamba hatutakubali kurudi nyuma, ya kwamba tutaendelea kufanya, hata iweje.
Hata mambo yangekuwa magumu kiasi gani, bado tutaendelea kufanya.
Kwenye kila changamoto tunayokutana nayo, tunaangalia kipi kizuri cha kufanyia kazi. Maana kila changamoto huwa inakuja na fursa zake.
Tutafanya chochote kitakachowezekana, kuhakikisha tunakamilisha mipango yetu, kuhakikisha tunafikia ndoto zetu.
Na hatutakubali mtu au kitu chochote kituzuie sisi kufanikiwa.
Jiambie I WILL DO WHATEVER IT TAKES, kwamba utafanya kila kinachowezekana kufanyika kuhakikisha unafika pale unapotaka kufika.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT