Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

IMG_20170102_073855
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tutaweza kufanya makubwa sana siku ya leo.

Asubuhi ya leo tutafakari nafasi ya nafsi zetu katika maamuzi tunayofanya kila siku.
Ndani yetu tunao uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi bora,
Tunao utashi ambao una uelewa mkubwa sana.
Na wakati mwingine utashi huu unajua jibu sahihi lakini haujui kwa nini jibu hilo ni sahihi.
Kuna wakati unaweza kuwa hujisikii kabisa kufanya jambo, lakini hujui kwa nini hujisikii. Ukaamua tu kufanya jambo hilo na mwishowe unapata matokeo mabovu.
Huu ni uwezo mkubwa ambao upo ndani yetu, japo huwa hatuupu nafasi.

Asubuhi ya leo tuangalie uwezo huu kwenye kutuzuia kutapeliwa au kuingia kwenye fursa ambayo siyo nzuri.
Unaweza kuelezwa kitu na kwa fikra zako ukaona haiwezekani ikawa kweli, yaani ni TOO GOOD TO BE TRUE, kila ukiangalia utamu wa maneno unayoambiwa, unaona haiwezekani kabisa.
Lakini wanaokuambia huwa ni wajanja, na wanajua utakuwa na wasiwasi, hivyo wanakuja na kauli kama, ona wenzako hawa wanafanya na wamenufaika, au usipochukua hatua sasa umeikosa fursa.
Kwa kauli hizo unaingia na mwishowe unaumia.

Ninachotaka uondoke nacho hapa asubuhi ya leo rafiki yangu ni hiki, ukishaanza kukitilia mashaka kitu, basi usikimbilie kufanya maamuzi, badala yake jipe muda wa kukichunguza kwa undani zaidi.
Sisemi ukikatae, maana pia unaweza kuwa unakosea, ninachosema ni jiridhishe, bila ya shaka yoyote ndipo uingie.

Kama kitu ni kizuri sana kuwa kweli, basi mara nyingi siyo kweli. Fanya homework yako, chunguza kwa makini na usikubali kupelekwa haraka kwenye maamuzi.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.