Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Hongera kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni fursa kubwa na ya kipekee kwetu kwenda kufanya yale tuliyopanga kufanya.

IMG_20170102_073855
Tutumie muda wetu wa leo vizuri, kwa sababu ukishapita haurudi tena.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kuDISCONNECT…
Tuna fursa ya kipekee ya kuishi zama hizi ambapo tumeunganishwa na dunia nzima, masaa 24 kwa kifaa kidogo sana ambacho kinaenea kwenye mkono wako.
Ni fursa kubwa sana kwa sababu hakuna tena mipaka, unaweza kufanya biashara na mtu yeyote duniani na pia unaweza kupata taarifa na maarifa kutoka sehemu yoyote duniani.
Lakini pia fursa hii inakuja na changamoto zake, ambapo kwa kuwa connected masaa 24 inachangia kupoteza muda na kushindwa kuweka vipaumbele vyako vizuri.
Mara nyingi unajikuta umeunganishwa na vitu ambavyo siyo muhimu kwako.
Lakini unashindwa kuondokana navyo kwa hofu ya kupitwa. Unaona usipokuwa connected basi utapitwa na mengi mazuri.

Asubuhi hii nataka ujikumbushe ya kwamba, unahitaji muda na wewe binafsi, muda ambao hauna usumbufu na muda ambao unaweka juhudi na maarifa makubwa kwenye kazi yako muhimu.
Na muda huu ili uweze kuufaidi vizuri, unahitaji kudisconnect.
Kuwa na muda wako binafsi, ambapo unajitenga na kelele za dunia ili uweze kufanya yako. Unaweza kuwa muda mfupi, lakini kama utautumia vizuri utaweza kufanya makubwa.
Na pia, hakuna chochote kitakachokupita.
Ondokana na dhana kwamba utapitwa,
Huhitaji kuendelea kuwa kwenye kila kundi la wasap ambapo upo sasa,
Huhitaji kutembelea kila mtandao wa kijamii kila saa kuona nini kinaendelea.
Hihitaji kujibu kila ujumbe na kupokea kila simu inayoingia kila wakati.
Muda wako mwenyewe ni muhimu sana, jitenge ma dunia na fanya yako. Mengine yote yanaweza kusubiri, wakati unafanyia kazi ndoto yako kuu.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako, Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.