Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho tumechagua kufanya.

Tutumie nafasi ya leo vizuri ili tuweze kupata matokeo bora kabisa.
Ni kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunaweza kufanya makubwa kabisa.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MISINGI NA WATU…
Kuna vitu hivi viwili ambavyo tunaweza kuamua tufuate kipi,
Unaweza kuamua kuwafuata watu, kufanya kile wanachofanya, hata kama siyo sahihi kwako kufanya,
Au unaweza kuamua kufuata misingi, ambayo imedhibitishwa kuleta matokeo bora.
Sasa watu wengi wamekuwa wanaachana na misingi na kufuata watu, na watu wale wanapopotea, wanapotea na wengi.
Ninachotaka ufanyie kazi rafiki yangu, ni kuacha kabisa kufuata watu na kuanza kufuata misingi,
Sisemi usikae na watu, bali ninachosema fanya kitu kwa sababu ni sahihi kufanya na kuna matokeo utapata, usifanye kitu kwa sababu kila mtu anafanya, au kwa sababu mtu fulani unayekubaliana naye anafanya.
Ukishaanza kuona unapata msukumo wa aina hiyo, ni wakati wa kukaa chini na kuanza kujimulika, misingi umeiacha wapi?
Uzuri ni kwamba utakapofuata misingi, utakutana na wengine ambao nao wanafuata misingi, na mtakwenda pamoja.
Watu wanaweza kuteleza, na kika mtu anatekeza, lakini misingi inabaki imara.
Ukiijua misingi na kuiishi, hakuna kitakachokupoteza,
Utakutananna changamoto, hiyo ni kawaida, lakini utakuwa unajua unakokwenda na uhakika wa kufika pale.
Kila kitu kwenye maisha yetu kina misingi yake,
Maisha yenyewe yana misingi,
Kazi zina misingi,
Biashara zina misingi,
Mahusiano yana misingi,
Dini zina misingi,
Siasa zina misingi,
Kitu chochote unachojihusisha nacho kwenye maisha yako, hakikisha unaijua misingi kwanza na kuifuata, hakuta atakayekubabaisha.
Wanaobabaishwa wote, wanaodanganywa na kitapeliwa, hawafuati misingi.
Fuata misingi, utakwenda vizuri.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.