Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

Leo hii tunakwenda kuweka NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ili tuweze kupata matokeo bora kabisa.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu maisha no safari.
Wengi wamekuwa wakitumia sana kauli hii kwamba maisha ni safari,
Lakini sijui kama awanaelewa maana yake, maana wanachosema hakiendani na wanachofanya.
Kwenye safari kuna kusogea, huwezi kusema upo safarini wakati kila siku upo pale ulipo.
Lazima uwe unasogea, kwa kiasi fulani, hata kama ni kidogo, ndiyo maana ya safari.
Sasa kama wewe upo pale pale miaka yote, haiwezekani hiyo ikawa safari,
Wewe upo kwenye kazi yako kwa miaka kumi, na hakuna mabadiliko yoyote.
Au upo kwenye biashara yako miaka kumi, lakini upo hivyo hivyo miaka yote, biashara ipo hivyo hivyo, haikui wala kuzaa nyingine.
Hapo sasa haupo safarini, labda umeamua kupumzika kwenye kituo cha safari.
Tunaposema maisha safari lazima yawe yanaakisi safari, kwenye kila eneo. Lazima uwe unapita kwenye maeneo mbalimbali kwa nyakati mbalimbali, ulichofanya jana, leo ufanye kwa ubora zaidi.
Safari ni mabadiliko, hivyo hakikisha maisha yako yana mabadiliko kila siku.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.