Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.

img-20161217-wa0002
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu DRAMA….
Usipokuwa makini kwenye haya maisha, kila siku utajikuta kwenye DRAMA, labda za kuanzisha wewe mwenyewe au wanazoanzisha wengine.
Drama tunayozungumzia hapa ni pale mtu anapokosa kitu cha kufanya, na kuamua kuibua mambo ili tu na yeye aonekane kuna kitu anafanya, au angalau hafanyi kwa sababu kuna kitu kinamzuia.

Drama hizi hazina mchango wowote kwenye mafanikio, hazizalishi chochote, bali tu zinafanya mtu aonekane naye yupo.
Ni moja ya vitu ambavyo wengi wanatumia kupoteza muda wao na wa wengine pia. Na wakati mwingine unajiona unasaidia kumbe umepotezwa na hizo drama.

Njia pekee ya kuondokana na drama, ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako, ni kuondokana kabisa na kila aina ya drama.
Kwa drama zako binafsi, epuka.
Ukishaanza kuona unafanya vitu ili watu wakuone, jua umeanza kuingia kwenye drama.
Kama unafanya kazi ambayo huipendi, na hivyo kuanza kutafuta sababu za kutokuwa kazini, labda kusingizia unaumwa au una msiba, jua tayari upo kwenye drama, ondoka haraka

Kwa drama za wengine, kaa nazo mbali sana.
Ukiona yupo mtu ambaye matatizo hayaishi kwake, jua hizo ni drama. Leo kaumwa, ugonjwa ukiisha anapoteza kitu, hajakaa sawa katapeliwa, anarudi tena kuumwa. Yaani kila wakati ni nyie kuweka macho kwake tu. Huyo yupo kwenye drama na anataka wote mcheze drama yake.
Wakati mwingine mambo yanatokea kweli kabisa, mtu anaumwa kweli kabisa, lakini ni drama, maana mwili wake unampa kile anachotaka.

Epuka kabisa hizo dramaa, hakikisha kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako ni kufanyia kazi ndoto yako kubwa. Usipoteze nguvu nyingi kwenye drama,
Tatizo la drama huwa naziishi, ikiisha moja inaibuka nyingine.
Hivyo usisubiri mpaka ziishe, badala yake kimbia haraka sana.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.