Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa na kupata matokeo makubwa zaidi.

Mwongozo wetu wa leo na kila siku ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kujificha.
Kwenye hii dunia, unaweza kufanya kazi bora kabisa, au unaweza kujificha.
Kufanya kazi bora kunakuhitaji wewe kuondoka kwenye kundi, kufanya kinyume na matarajio ya wengi na kufanya kile ambacho wengine hawapo tayari kufanya.
Kufanya kazi iliyobora kunakuweka hadharani kwa kukosolewa, kupingwa na kukatisha tamaa. Ni jambo ambalo linaogopesha na linahitaji ujasiri makubwa.
Kujificha ni pale unapoweka pembeni kufanya kazi iloyo bora, na kufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Unafanya kama unavyotarajiwa kufanya na hakuna kikubwa au cha tofauti unachofanya.
Unajificha nyuma ya kazi yako ya kila siku, kila asubuhi unaamia na kwenda kazinim kufanya kile unachofanya kila siku, kurudi nyumbani na kesho unarudia tena.
Unajificha kwa kufanya biashara yako kwa mazoea, kuwa pale pale unapokuwepo mara zote.
Kujificha no rahisi, maana hakuna anayekuona wa tofauti, hakuna wa kukupinga wala kukukosoa.
Kuwa ndani ya kundi kubwa ni kujifucha.
Huwezi kufikia mafanikio makubwa kama utaendelea kujificha.
Acha sasa kujificha na chukua hatua, fanya kwa utofauti na usijali kuhusu watakaokukosoa au kukupinga, watapita na hakuna atakayekuja kuwakumbuka, ila wewe utakumbukwa kwa makubwa uliyofanyq.
Anza kufanya leo, acha kujificha.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.