Habari rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ili tuweze kupata matokeo bora sana.

img-20161217-wa0002

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUFIKIRI UNACHOFIKIRI.
Kama ipo kazi ngumu sana hapa duniani, basi kazi hiyo ni kufikiri.
Kufikiri ni kugumu ndiyo maana wengi huwaachia wengine wawafanyie kazi hiyo.
Tafadhali usichanganye kufikiri na kuwa na mawazo, kuwa na mawazo ni rahisi, huhitaji hata kuweka juhudi, ila kufikiri na hasa kufikiri kwa kina, ni kazi nzito.

Sasa ukiacha tu kufikiri, kuna kufikiri juu ya unachofikiri. Maana wakati mwingine unaanza kufikiri na fikra zako zinapotea njia, unajikuta unafikiri kitu ambacho hukupanga kufikiri na hakiwezi kukusaidia.
Ili kuhakikisha fikra zako zipo eneo sahihi, unahitaji kufikiri juu ya unachofikiri, mara kwa mara.
Unahitaji kujihoji juu ya kile unachofikiri muda mwingi, ukizingatia na maono makubwa ya maisha yako, je ni vitu ambavyo vinaendana?

Kufikiri juu ya kile unachofikiri ni njia ya kujizuia kupotea, kwa sababu wengi hupotea mpaka pale wanapopata matokeonya tofauti ndiyo wanagundua hawakuwa wakifikiri sawa sawa.

Leo nenda kafikiri juu ya unachofikiri muda mwingi.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.