Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

Siku ya leo tunaiendea tunaiendea kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu ANAYEAHIDI KILA KITU,
Huyu, hakuna chochote anachoahidi.
Yaani mtu anayeahidi kila kitu, hakuna anachoahidi,
Kwa sababu kadiri mtu anavyoahidi mengi, ndivyo inavyokuwa ngumu kwake kutekeleza na hivyo kutokutekeleza kabisa.
Hivyo unapoona mtu anaahidi mengi, usipoteze muda wako kusubiri atimize anayoahidi, hawezi kutimiza. Na kadiri anayoahidi yanavyokuwa mengi, ndivyo uwezekano wa kutimiza unavyokuwa mgumu.
Kwa upande wako pia, unapojikuta ukiahidi mengi, jua kabisa hutaweza kuyatekeleza. Jua tu unawapa watu matumaini ya uongo.
Na muhimu zaidi, jua unaharibu jina na sifa yako, unakuwa mtu anayetoa ahadi za uongo.
Kuna wakati unaweza kuwa unakitaka sana kitu hivyo kusukumwa kuahidi kila kitu ili upate unachotaka, ninachokuambia, usikubali kufanya hivyo.
Madhara yake ni makubwa sana baadaye.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.