Ni siku nyingine nzuri sana ya leo rafiki,
Siku ambayo jana uliita keshom na kujiambia yapo mambo ambayo ungeyafanya leo hii.

IMG_20170102_073855
Nakukumbusha tu kesho uliyoisema ndiyo leo na hivyo hakikisha unafanya ulichosema, usije kuahirisha tena leo.
Leo nenda kaweke juhudi kubwa ili uweze kupata matokeo makubwa.
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo utaweza kufanya makubwa sana.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kufanyw zaidi,
Najua unajua, lakini kukumbushana ni muhimu zaidi.
Huwezi kutoka hapo ulipo sasa, kwa kuendelea kufanya vile unavyofanya sasa.

Yaani kabisa unafikiria utaondoka kwenye hiyo kazi kwa kuendelea kwenda kazini asubuhi, kufanya kazi zako kama kawaida na kurudi nyumbani?
Au utoke hapo kwenye hiyo biashara ambayo unauza vitu vile vile kwa wateja wale wale, eneo lile lile na kwa mbinu zile zile?
Au uelewa wako ubadilike huku hakuna kipya unachojifunza?

Haihitaji shahada au wafadhili waje kukuambia kwamba ukifanya kile ambacho umezoea kufanya, utaendelea kupata matokeo uliyozoea kupata.
Kupiga hatua, lazima kwanza ubadili kile unafanya, lazima ubadili mtazamo, lazima uwe na uelewa mkubwa zaidi.

Ndiyo maana ni muhimu sana kufanya zaidi, fanya zaidi ya ulivyozoea sasa, fanya zaidi ya unavyotegemewa, wafikie wengi zaidi na toa vingi zaidi ya unavyotoa sasa.
Ukuaji unaanza na kufanya zaidi.
Acha kufanya kwa mazoea,
Kila siku hakikisha kuna hatua ya tofauti unaipiga, ya kwenda mbali zaidi.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.