Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

IMG_20170102_073855
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo utaweza kufanya makubwa sana.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTUMIA VIZURI WAKATI KIPO.
Chochote ulichonacho sasa, kuna siku hutakuwa nacho,
Yaani vitu tunavyovichukulia kwa kawaida leo, kuna siku vitaondoka.
Na inapofika siku hizo ndipo wengi husema ningejua….
Sasa wewe huna haja ya kusubiri mpaka viondoke ndiyo useme ungejua.
Badala yake unahitaji kutumia vizuri kila ulichonacho leo, maana hujui kama kesho utakuwa nacho.
Tumia vizuri leo ili hata kama kesho hutakuwa nacho, ujue ulitumia vizuri wakati ulikuwa nacho.

Na hii ni kwa kila kitu,
Kuanzia afya yako, nguvu zako, muda wako, watu wanaokuzunguka, kazi, biashara na kila kitu kinachokuhusu leo.
Na hata kama ukichonacho hakitaondoka, basi kumbuka hutaishi milele.
Hivyo fursa kama hii uliyopata leo, itumie vizuri.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.