Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Hii ni fursa ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.

Tutumie muda wetu wa leo ili tuweze kufanya makubwa.
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambazo ndiyo nguzo muhimu kwa mafanikio yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MATOKEO GANI UNATARAJIA?
Kwenye kitu chochote unachofanya, usianze tu kufanya kwa sababu unataka kufanya, au kwa sababu muda wa kufanya umefika.
Badala yake pata kwanza picha ya matokeo unayotaka kufanya.
Anza na ile picha ya mwisho kwenye akili yako.
Ona ni kipi unataka kukamilisha, kipi unataka kufanya na matokeo gani unayotaka kutoka nayo.
Kwa kuanza hivi utakuwa na uelewa wa wazi kipi unapata na wapi upite.
Lakini kama utaanza kuparamia na kufanya vitu, mida utakwenda, utajiona umechoka lakini matokeo uliyopata huyaoni au huridhishwi hayo.
Hiyo ni kwa sababu ulikuwa unafanya ili tu kufanya na siyo kwa sababu ya maono uliyokuwa nayo.
Chochote unachotoa muda wako kufanya, hakikisha unajua kwa hakika ni wapi unataka kufika na ni matokeo gani unataka kupata. Tofauti na hapo unakuwa umechagua kupoteza muda na nguvu zako.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.