Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.

Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao unatuwezesha kifanya makubwa kila siku.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu HUJUI HUJUI…
Kikwazo kikubwa kwa kila mtu kufanikiwa, au kupata kile anachotaka kinaanzia kwenye vile vitu ambavyo mtu hajui.
Usichojua ni kikwazo kwako kifanikiwa, kwa sababu kinakurudisha nyuma kwenye hatua ambazo ulitaka kupita.
Yaani, kile ambacho ni muhimu kwako kupiga hatua, halafu hukijui, kitakuwa kikwazo kwako kufanikiwa.
Sasa vipi vitu ambavyo TUNAJUA HATUJUI, hivi havina shida sana kwa sababu tunaweza kuvifanyia kazi. Si tunajua hayujui, hivyo tunaweza kuchukua hatua ya kujua.
Hatari kubwa ipo kwenye vile vitu ambavyo HATUJUI HATUJUI,
Yaani hujui kitu, halafu hujui kwamba hukijui. Hivyo wewe utaendelea na maisha yako kama kawaida, huku ukiona kila kitu kipo sawa, kumbe kuna kizingiti kikubwa ambacho hata hukijui.
Ili kuondokana na kuzingiti hicho, ni muhimu sana kujifunza mambo mapya kila siku. Kila siku jifunze kitu kipya, kupitia wengine na kupitia unachofanya.
Usikubali siku ipite hujajifunza.
Pia chagua watu ambao wamefanikiwa sana kwenye hicho unachofanya, na angalia ni vitu gani wanafanya ambavyo wewe hufanyi.
Hii itakuwa njia rahisi kwako kijua vile ambavyo hujui.
Usijifungie mwenyewe na kufikiri unajua kila kitu.
Vipo viti vingi ambavyo hujui na pia kujui kama hujui.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.