Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwends kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Tutumie muda wetu wa leo vizuri ili tuweze kufanya makubwa.
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MGODI WA ALMASI….
Watu wengi wamekuwa wakizunguka sana kutafuta wapi wanaweza kupata mgodi wa almasi, au mgodi wa dhahabu. Ili wakishaupata kazi yao ni kuchimba tu na kupata fedha nyingi.
Wapo ambao wanapata hiyo migodi na wapo ambao hawaipati.
Na katika wale wanaopata migodi ya almasi, wengi haidumu, baada ya muda mgodi unakauka na hivyo kuendelea tena kusaka mgodi mwingine.
Kitu ambacho wengi hawajui ni kwamba, pale walipo, wanatembea na mgodi wa almasi, tena almasi yenye thamani kubwa na isiyoisha kamwe. Mgodi huo wameubeba wao wenyewe na wanaenda nao kila mahali, ila wanashindwa kuutumia, kwa sababu hawajui kama upo, na hata wakijua, hawajui wanawezaje kuutumia.
Mgodi wa almasi unao hapo ulipo sasa, na upo ndani ya kichwa chako,
Mgodi wa almasi ni ubongo wago, na almasi yenyewe ni akili yako.
Ukiweza kuitumia vizuri akili yako, utapata chochote unachotaka kwenye maisha yako.
Kwa sababu unachopata ni matokeo ya fikra zako.
Hivyo rafiki, acha kuhangaika huku na kule ukitafuta mgodi wa almasi,
Au kwa lugha ya sasa, kuzunguka kutafuta fursa.
Fursa ya kwanza kabisa uliyonayo ni akili yako, itumie vizuri na utaweza kufanya makubwa.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.