Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Ni siku nyingine nzuri ambayo tuna nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.

img-20161217-wa0002
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.
Na kauli yetu ya mwaka huu 2017 ni KUTHUBUTU, USHINDI NA SHUKRANI, ambapo leo hii tutakwenda kuthubutu mambo mapya, tutapata ushindi na kushukuru kwa kila jambo.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu UNAPOZAMA….
Hakuna wakati mzuri wa kujifunza kuogelea kama wakati unapozama.
Maana hapo huna namna nyingine bali kujiunza kuogelea ili kuokoa maisha yako.
Hata kama hujawahi kuogelea kabisa, ukitupwa kwenye maji na kuanza kuzama, lazima utajifunza kuogelea. Hii ni kwa sababu hutakuna na cha kukusubirisha tena, ni uchukue hatua upone, au usubiri na ufe.

Wakati wa matatizo unatupa fursa kubwa ya kujua nini hasa tunaweza. Bila ya matatizo tunafanya yale tuliyozoea kufanya, na hatuna haraka ya kufanya makubwa zaidi. Lakini unapokuwa kwenye hali kwamba huna namna, lazima utafanya yale makubwa.

Matatizo yanatupa fursa ya kujua uwezo mkubwa ambao upo ndani yetu. Wakati mwingine yanatuwezesha kujua nini tunajua, maana tunakuwa tunachukulia ni kawaida kwa kuwa hatujapata matatizo.

Hivyo rafiki, hapo ulipo kuna makubwa sana unaweza kufanya, sema hujasukumwa na matatizo au mazingira kulazimika kufanya hayo makubwa.
Pia unapopitia matatizo, usikimbilie kukata tamaa, bali angalia ni hatua zipi unazoweza kuzichukua kwenye maisha yako ili mambo yaweze kuwa vizuri.
Usikubali kirahisi, PAMBANA, kama ambavyo hungekubali kuzama kirahisi.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.