Kinachofanya watu wachukie uzee siyo tu hali mbaya ya afya, bali kuwa na uhakika kwamba kifo kimekaribia.
Watu wengi wanaogopa sana kifo kwa sababu kuu mbili;
1. Kutokuwa na uhakika nini kitatokea baada ya kifo.
2. Kuhofia kwamba mtu hajayaishi maisha yake, hivyo kuhitaji muda zaidi ili kuyaishi maisha.
Wastoa wanasema kwamba kifo hakipaswi kuogopwa wala kukimbiwa, bali kinahitaji kukaribishwa vizuri.
Kama umeyaishi maisha yako vizuri, na kufanya kile hasa unachopaswa kufanya, huna sababu ya kuogopa kifo.
Wastoa wengi walikuwa na vifo vya kuadhibiwa au kujiua wenyewe.
Na hawakuhofia vifo hivi kwa sababu walishayaishi maisha yao.
Musonium anasema kwamba ni bora kufa vizuri kama ukiweza kupata fursa hiyo, kuliko kusubiri na ukaikosa.
Sisi kama wastoa, hatupaswi kufikiria sana kuhusu kifo, na pale umri utakaposogea, tusihofie kifo, badala yake tukazane kuishi maisha yetu, na wakati wetu utakapofika, tuukaribishe.