Seneca anasema, watu hawana furaha kwa sababu hawajui hasa ni nini wanataka kwenye maisha yao. Wanakazana kutafuta umaarufu wakiamini wakiwa nao watakuwa na furaha, lakini kila umaarufu una gharama zake.

Kwanza kabisa unapotaka wengine wakukubali, maana yake inabidi ufanye yale wanayotaka wao. Na hivyo huwezi kuishi maisha yako, hivyo hata ukiwa maarufu, hutakuwa na furaha.

Epictetus anasema umaarufu una gharama ya kulipa na gharama hiyo ni kuacha maadili yako binafsi na kubeba madili ya wengine, ambayo yanaweza yasiwe na maana kwao.

Kutaka umaarufu ka wengine pia kunakuondokea wewe uhuru wako, unapofanya kitu ili uonekane au usifiwe na wengine, hupo huru.

Marcus Aurelius anatuambia tusipoteze muda wetu kufikiria wengine wanatufikiria au kutuchukuliaje. Badala yake tufanye yetu, tuwe na maadili yetu na tuyaishi.
Kulazimisha usifiwe au ukifa jina lako libaki ni kupoteza muda. Badala yake unapochagua kugaishi maadili yako, hasa maadili ua ustoa, utajikuta unakuwa maarufu bila hata ya kulazimisha.
Watu watapendezwa na namna maisha yako yanavyokwenda na hivyo kuwa maarufu zaidi.