Moja ya vitu vinavyowavuruga watu ni kukazana sana kutafuta fedha ili kuishi maisha ya anasa. Kuweza kuvaa nguzo nzuri na zinazowavutia wengine, pia kula vyakula vitamu ba kuishi majumba ya kifahari.
Kutaka na kupata vitu vizuri siyo kubaya iwapo dhamira ya moyo wetu ipo safi. Lakini kama tunafanya ili tu tuwe na maisha ya anasa, tutajiumiza sana.
Na hii ndiyo imepelekea unakuta mtu anacho kila anachotaka lakini hana furaha, maisha hayana maana kwake.
Wastoa wanatushauri kwamba, tusikimbizane na fedha ili kuwa maarufu au kuishi kwa anasa. Badala yake tuishi maisha yetu ya kawaida kulingana na maadili yetu.
Wastoa wanatuambia;
Tuke chakula ili kuishi na siyo kula kwa sababu ya utamu wake.
Tuvae mavazi kwa ajili ya kusitiri miili yetu na siyo kuwaonesha wengine kwamba tuna mavazi mazuri.
Tukae kwenye nyumba zinazotuoa hifadhi na siyo kwa sababu ni za kifahari.
Wastoa wanatuambia hakuna sumu mbaya kama kuzoea maisha ya kifahari, kwani unasahau kabisa ulipotoka na siku mambo yakienda vibaya, unakuwa na maisha ya mateso sana.
Kwa kuishi kwa msingi huu wa ustoa, haimaanishi tukatae utajiri, au tupende umasikini, badala yake tusiwe watumwa wa utajiri.
Kwa kuishi hivi tutaweza kufikia utajiri mwema, wenye maana kwetu na kwa wengine pia. Kama wastoa Seneca na Marcus Aurelius walivyoweza kuwa matajiri wakubwa.
Tusilewe na maisha ya anasa, bali tuishi maisha ya msingi kwetu na mengine yatakwenda vizuri.