Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kupata matokeo makubwa.

IMG_20170102_073855
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NEVER DROP OUT….
Maisha yana changamoto, hilo halina ubishi,
Siyo mara zote utapata kile ambacho unataka.
Na wakati mwingine utafanya kila unachopaswa kufanya, lakini matokeo yanakuja tofauti kabisa na ulivyotegemea.
Hapa ndipo wengi hukata tamaa na kuona kama waliweka juhudi kubwa kiasi kile lakini hawajapata matokeo mazuri, kipi tena wanaweza kufanya?
Kwa fikra hizi mtu anaamua kiacha, ana DROP OUT.

Yapo mambo ambayo unaweza kudrop out, lakini inapokuja kwenye ndoto yako, kwenye maono yako makubwa ya maisha, NEVER DROP OUT.
Kamwe usiache kukimbiza ndoto yako hata kama kila njia unayojaribu unakwama.
Kamwe usiache kwa sababu dunia nzima inapingana na wewe, kwa sababu hakuna aliyewahi kufanya.

Mambo yote yaloyoleta mapinduzi duniani, mwanzo yalipingwa sana, hata ndege tunazofurahia leo, waliokuja na wazo la kutengeneza ndege walionekana kama wana ugonjwa wa akili.
Hivyo wewe unajua zaidi ya mtu yeyote yule kuhusu ndoto yako.
Ifanyie kazi na NEVER DROP OUT, hata kama utakutana na magumu kiasi gani.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.