Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana.

img-20161217-wa0002
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTEGEMEA USICHOTEGEMEA….
Kila mtu ana mategemeo na matarajio fulani kwenye maisha, na kwenye kila anachofanya.
Kila mtu kuna kitu anategemea kitokee, pale anapoweka juhudi kubwa.
Na mara zote huwa ni mategemeo ya kile kilicho bora, mategemeo ya mambo mazuri.

Lakini uhalisia haupo hivyo, ni mara chache sana unapata kile unachotazamia kupata. Mara nyingi unapata matokeo tofauti kabisa ambayo hata hukuyategemea.
Hali hii huwaumiza wengi na kuwavunja moyo, na kuona hawawezi kupata makubwa wanayotegemea tena. Hivyo hukata tamaa na kutochukua tena hatua.

Kukata tamaa siyo jibu, kwa sababu hata kwa kufanya hivyo, bado hupati kile ambacho ulikuwa unategemea kupata.
Hivyo basi, ili kuondokana na hali hii, anza kwa kutegemea usichotegemea. Ni vizuri kuwa na mategemeo mazuri na makubwa, lakini pia kwenye akili yako usisahau kuna matokeo tofauti na uliyotegemea.
Jua kipi tofauti kinaweza kutokea na jua kabisa utakitumiaje kupata kile unachotaka wewe.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.