Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao ndiyo msingi wa mafanikio yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu TABIA NA AKILI….
Hivi ni vitu viwili ambavyo ni muhimu sana kwa mafanikio.
Kukosa vyote viwili kunakuzuia kufanikiwa kabisa,
Na kuwa na kimoja kunafanya mafanikio yawe kidogo.
Tabia ndiyo inayopelekea wewe kufanya au kutokufanya mambo fulani.
Tabia ndiyo inawapelekea watu kukuamini au kutokukuamini.
Na tabia ndiyo inakujenga wewe kama mtu, watu wanakujua wewe kwa tabia zako.
Akili ndiyo inakuwezesha wewe kuziona fursa za mafanikio zinazokuzunguka.
Akili ndiyo inakuwezesha wewe kuzitumia fursa hizo vizuri kwa mafanikio yako.
Na akili ndiyo inakuwezesha kuvuka changamoto na vikwazo vinavyoweza kukuzuia kufanikiwa.
Hivyo rafiki, unahitaji sana vitu hivi viwili,
Fanyia kazi tabia zako, jenga tabia bora za mafanikio, tabia za kufanya kazi kwa juhudi, kujituma, kuheshimu wengine, kujali muda.
Na pia ijenge akili yako kwa kufikiri kwa kina, na kuilisha akili yako maarifa bora kabisa kupitia vitabu vizuri vya mafanikio.
Usishindwe kufanikiwa kwa sababu ya vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wako kabisa.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info