Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwends kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.


Msingo wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunaweza kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTEGEMEWA…
Kwenye dunia, watu huwa wanaheshimu kile ambacho wanakitegemea na kudharau kile ambacho hawakitegemei.
Kile ambacho watu wanakitegemea kweli wanakipa heshima kubwa kwa sababu wanajua hawana namna nyingine.
Na hili ndiyo swali kubwa kwako kutafakari asubuhi ya leo, JE UNATEGEMEWA KWA LIPI?
Ni vitu gani ambavyo watu wanategemea kwako?
Ni nini ambacho watu hawawezi kupata kwingine ila kwako tu?
Ni mambo gani ambayo kama wewe hupo itabidi yasubiri?

Na hii ni kwenye kila unachofanya kwenye maisha yako,
Iwe ni kazi, kama hakuna unachotegemewa nacho kwenye kazi yako, hakuna atakayehangaika na wewe.
Hata kwenye biashara, kama hakipo kitu ambacho wateja wanakipata kwako tu, hakuna atakayehangaika na wewe.
Na hata kwenye maisha kwa ujumla.
Kutegemewa hapa siyo kwa misaada, bali kwa kile unachofanya, ambacho hakiwexi kufanywa pengine.

Ongeza thamani yako leo kwa kutengeneza utegemezi wz watu kwako, kwa kufanya vitu ambavyo watu hawawezi kuvipata pengine ila kwako pekee.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info