Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya nakubwa sana leo na kila siku.
Asubuhi ya leo tunatafakari kuhusu APP na NIDHAMU…
Tangi tumekuwa na hizi simu janja (smartphone) kuna programu (applications) za kila kitu, KILA KITU.
Kuanzia kudhibiti muda, kusoma, kujisimamia mwenyewe, fedha, mazoezi, mawasiliano na kila kitu, kasoro labda app ya kupakua chakula.
Tangu tumekuwa na uwezo huu wa kuwa na app yoyote tunayoitaka, tumehamisha tatizo kutoka kwenye NIDHAMU BINAFSI na tatizo kuwa APP NZURI.
Sasa hivi mtu akitaka kufanya kitu, anajiuliza app gani itamfaa.
Na mtu akishindwa kufanys kitu, atasingizia hajapata app nzuri.
Hata watu wanapoomba ushauri kwa wengine, hutaka kujua app gani wanazotumia zinazowawezesha kufanikiwa.
Fikiria hili rafiki,
Siyo app inayokuwezesha kufanikiwa au kukuzuia,
Bali nidhamu binafsi, ya kufanya, kile ulichopanga kufanya, kwa wakati uliopanga kufanya, ndiyo itakuwezesha kupiga hatua.
Unaweza kuwa na app ya kils sina, lakini kama nidhamu binafsi hakuna, app hizo hazina msaada wowote.
Kwa mfano unaweza kuwa na app ambayo inakuwezesha kupangilia muda wako vizuri, lakini bado unahitaji wewe uchukue hatua kuhakikisha unatumia muda wako.
Au ukawa na app inayoonesha ni mazoezi kiasi gani umefanya, lakini lazima wewe ufanye mazoezi. App haitakubeba na kukufanyisha mazoezi.
Hivyo rafiki, tusijaribu kuhamisha tatizo ili kuondoa lawama kwetu, app siyo suluhisho, ni njia tu. Suluhisho ni NIDHAMU BONAFSI, Uwezo ea kufanya kile ulichopanga kufanya, kwa wakati uliopanga kufanya, iwe unajisikia kufanya au la.
Ukishajijengea nidhamu binafsi, ndipo apps zitakuwa na msaada kwako.
Vinginevyo zitakuwa na mzigo tu unaojaza nafasi kwenye simu yako.
Usikimbizane na apps, jenga nidhamu binafsi.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info