Watu wote ambao wanaingia kwenye biashara kwa msukumo wa kupata faida pekee, huwa hawadumu muda mrefu. Ni sheria ya dunia kwamba chochote ambacho hakipo kwenye misingi sahihi, kinaanguka. Wale wanaofikiria faida pekee, wanafanya kila wawezalo kupata faida, hata kama linaharibu mahusiano na wateja.
Kipimo kizuri sana kwako kuepuka hilo ni kujiuliza swali hili kila wakati unapomhudumia mteja wako. Je miaka 20 kutoka sasa, mteja huyo atakutafuta na kutaka kufanya biashara na wewe? Kama jibu ni ndiyo, unafanya kazi nzuri, kama jibu ni hapana, jiangalie vizuri.
Unaweka miaka 20 kwa sababu kwa kipindi hicho, kama kuna uongo wowote unakuwa umeshakuwa wazi. Kwa sababu kuna wakati watu huwezi kudanganya kwa muda, lakini baadaye mambo yote yanakuwa wazi. Iwapo unachofanya ni sahihi, na kina msaada kwa watu, watu wataendelea kukumbuka ulichowafanyia. Hivyo hata miaka 20 ikipita, bado watakuwa wanakufikiria wanapopata ile shida unayoweza kutatua wewe.
Mara zote toa thamani, mara zote wasaidie watu kuwa bora zaidi na mara zote timiza kile ulichoahidi mteja atapata akija kwako. Kwa njia hiyo utatengeneza wateja ambao wapo tayari kununua kwako tena na tena.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog
