Upo utafiti ambao uliwahi kufanywa ambao sio rasmi, ila utafiti huo una uhalisia ndani yake. Utafiti huo unasema ya kwamba, moja kati ya sababu kubwa za watu wengi kutokufanikiwa katika maisha yao, ni kwa sababu watu hao wamezoea kufanya vitu mbalimbali kimazoea, na kufanya hivyo kumewafanya watu hao kuelekea jehanamu ya umaskini.
Kwa mfano unaweza kukutana na mtu anapenda sana kufanya jambo fulani ambalo halina faida, na endapo utamuuliza mtu huyo mbona unapenda kufanya hivi kila wakati, utamsikia mtu huyu akinyanyau kinywa chake akisema, kitu hiki ndicho ulevi wangu, hii ikiwa na maana ya kwamba hawezi kufanya jambo jingine bila kufanya jambo hilo kwanza.
Kwa mfano huo hapo ndipo utakapojua ukweli ni kwamba watu wengi tunapenda sana kufanya vitu kwa mazoea, na kufanya hivi kunaturudisha nyuma sana katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo kama na wewe umezoea kufanya jambo fulani kimazoea ipo kanuni moja ambayo ni muhimu ya mafanikio, ambayo unatakiwa kuitumia katika maisha yako.
Na kanuni hii inakukumbusha wewe kila wakati kuweza kutengeneza tabia ya kwenda hatua ya ziada kwa kile unachokifanya. Kwa mfano, kama ni mtu wa kufanya kazi kwa saa nane, ongeza masaa mengine ya ziada kwa hicho unachokifanya, ukifanya hivi itakusaidia sana wewe kuweza kupiga hatua kubwa za kimafanikio.
Pia ikumbukwe ya kwamba mafanikio makubwa kila wakati yanakuja kwa kufanya zaidi ya pale ulipojiwekea. Acha kuishia pale kwenye mazoea yako ya kila siku. Nenda hatua ya ziada. Wataalamu wa masuala ya mafanikio wanakwambia GO EXTRA MILE. Kujituma hadi kufikia hatua ya ziada ni msingi mzuri sana wa kufikia mafanikio makubwa.
Hivyo endapo utajijengea utaratibu wa kufanya kazi pasipo kuendekeza mazoea utapata faida zifutazo:-
1. Kuweza kupata kile unachokihitaji.
2. Husaidia kuongeza ufanisi katika kazi.
3. Husaidia kupata mara dufu zaidi ya awali.
4. Mwisho utatengeneza amani ya moyo, kwani hiki ndicho kitu kikubwa ambacho kila msaka mafanikio lazima awe nacho.
Hivyo tumalizie kwa kusema ya kwamba kwa kila kitu ambacho unakifanya jifunze kuwa ni mtu wa kwenda hatua za ziada ili uweze kufanikiwa zaidi.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio tembelea dirayamafanikio.blogspot.comkujifunza na kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Website; www.amkamtanzania.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
