#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO.
KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems.
Kurasa 1 – 20.

Tiba ya akili ipo ndani yako.
Kitu ambacho sayansi inadhibitisha zama hizi, wanafalsafa walishakijua zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Hii ni kuhusu uwezo wa mtu kutibu akili yake mwenyewe.
Wanafalsafa wa kale, walitofautiana kwa misimamo mingi, lakini wote walikubaliana kwa jambo moja, kwamba tunakuwa kile tunachofikiri.
Kwamba maisha yetu yapo jinsi yalivyo, kutokana na mawazo yaliyotawala akili zetu.
Na hivyo tiba sahihi ya jambo lolote ambalo haliendi sawa kweye naisha yetu ni kuanza kubadili fikra zetu.
Kama unajisikia vibaya, unakata tamaa na kuona mambo hayawezekani, ni kwa sababu mawazo yaliyotawala akili yako yanasadifu hilo.
Dhana hii imekuwa ikitumika kuwatibu watu mbalimbali wenye matatizo ya afya ya akili, na imekuwa inaleta matokeo bora kabisa.
Hivyo basi, badala ya kukazana kutafuta tiba na suluhu ya matatizo na changamoto zetu kwa wengine, hebu kwanza tuanzie ndani yetu wenyewe, kwa kujenga fikra sahihi kwa kile tunachotaka.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa