KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 143 – 152.

Tumejifunza kutoka kwa wanafalsafa wa ustoa kwamba maisha yetu ni matokeo ya fikra zetu. Iwe ni furaha au huzuni, yote yanaanzia kwenye fikra zetu.
Lakini fikra zetu hizi zinaathiriwa na mazingira yanayotuzunguka.
Jamii tunazoishi na wale wanaotuzunguka, wana mchango mkubwa sana kwa fikra tulizonazo.

Wanafalsafa ambao wamechagua kuibadili jamii Cynics wanatuambia kwamba, ustaarabu ni mateso makubwa kwetu.
Hii ni kwa sababu kwenye maisha ya jamii, kuna mambo fulani watu wanalazimika kufanya ili waonekane wamestaarabika, japo kuwa mambo hayo hayana maana kabisa kwao.

Hapa ndipo wabafalsafa hawa wanotuambia tunapaswa kukataa hizo aina za ustaarabu na kuweka juhudi kuhakikisha tunaibadili jamii.

Cynics wamekuwa wakipambana na mfumo wa ubepari, wakiamini ni mfumo mbovu sana kwa uchumi, afa za watu na hata akili zao.
Wanasema kwenye mfumo huu wa ubepari, dunia imekuwa kama MBWA KULA MBWA, yaani kila mtu ni hatari kwa kila mtu.

Huenda hilo likafanikiwa, kwa mfumo kuvunjika wenyewe. Swali ni je ustaarabu huu ukivunjika, upi utachukua sehemu yake? Bila shaka utakuja mfumo mpya ambao unaweza kuwa mbaya zaidi.
Hakuna haja ya kujali hayo yajayo, muhimu ni kuchukua hatua sasa ili kuokoa kizazi na maisha ya dunia.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa