KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa; 177 – 186..
Mwanafalsafa Plato, kupotia kitabu chake cha The Republic, aliandika kwamba dunia itatulia na kuwa sehemu salama, iwapo wanafalsafa wataitawala dunia.
Aliamini changamoto ambazo dunia inipitia, zinaweza kutatuliwa na wanafalsafa pekee. Kwa sababu wao wanaijua misingi muhimu ya maisha.
Katika wazo lake hili, Plato alisema utawala umegawanyika kwenye makundi matatu;
Kundi la kwanza ni viongozi au watawala, ambao ndiyo wanaofikiri na kuwaongoza wengine.
Kundi la pili ni la wanajeshi, hawa wanapenda ushindi na utiifu.
Kundi la tatu ni la wafanyabiashara, hawa wanajali kuhusu fedha.
Plato anasema iwapo kundi la kwanza litaongozwa na wanafalsafa, basi jamii nzima itanufaika sana.
Ndoto hizi za Plato haziwezekani kwenye jamii kubwa ya watu, kwasababu ni vigumu sana kuwalazimisha watu wote kukubaliana kwenye jambo moja. Ndiyo maana tuna dini nyingi na hata vyama vingi vya siasa.
Njia bora ya wanafalsafa kuwafikia wengi ni kutengeneza mfumo wa kutoa mafunzo hayo ya falsafa kwa wale wanaowalenga.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa