KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans
UKurasa 217 – 226…
Wanafalsafa wa kigiriki waliamini kwamba kifo ni zoezi la kiimani.
Waliamini maisha yote tunayoishi, ni kujiandaa na zoezi kuu ambalo ni kifo.
Socrates alisema falsafa ni kujiandaa na kifo.
Seneca aliamini kwamba inachukua maisha yetu yote kujifunza jinsi ya kufa.
Marcus Aurelius alisema kifo ni sehemu ya maisha, na inapaswa kufanywa vizuri.
Ukweli ni kwamba hakuna atakayetoka hapa duniani akiwa hai, wote tutakufa na hivyo itakuwa vizuri kama tutakufa kifo kizuri.
Wanafalsafa wa kale waliamini kifo kizuri ni kile ambacho mtu amekikubali, kwamba amejiandaa na kujua hawezi kupingana na kifo, wakati ukiwadia umewadia.
Wanafalsafa hawa waliamini mtu anapokamilisha kazi yake hapa duniani, basi anakufa, bila ya kujali umri wake.
Hivyo yule anayetekeleza wajibu wake kwa wakati, anakufa kifo kizuri.
Ila yule ambaye hajafanya kile alicholetwa kufanya hapa duniani, anakufa kifo kibaya.
Kuna mengi kuhusiana na kifo, kidini na kiimani, lakini kama tutafuata ushauri huu wa wanafalsafa, ni vyema tukatekeleza wajibu wetu kwa wakati, kwa sababu hatujui ni wakati gani kwa hakika tutakufa, lakini tunajua tutakufa.
Tujiandae na kifo chema, kwa kutekeleza wajibu wetu kwa wakati.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa