KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 6 – 16.

Ukiangalia kwa undani falsafa zote za kale, kuanzia Ugiriki mpaka Roma, zina misingi yake kutoka kwa mwanafalsafa Socrates.
Socrates anaweza kuchukuliwa kama mwasisi wa misingi mingi ambayo falsafa nyingi zimejengwa juu yake.
Hata misingi ya baadhi ya dini, imetohoa baadhi ya mambo kwenye falsafa ya Socrates.

Watu wote waliofanikiwa, walioweza kufanya makubwa hapa duniani, wanakiri kwamba Socrates alikuwa hamasa kwao kufanya makubwa.
Sasa kama hawa waliofanikiwa katika zama hizi ni mamenta wetu, na wao wanamchukulia Socrates kama menta, hii inamfanya Socrates kuwa menta wa mamenta.

Pamoja na kuonekana kuwa mtu anayejua sana, mara zote Socrates alisema kitu kimoja, hajui. Kutokujua kwake ndiyo kulimfanya awe na kiu ya kujifunza zaidi na zaidi.
Mtindo wa kujifunza na kufundisha wa Socrates ulikuwa wa kuhoji. Alipenda majadiliano na kuhoji maswali mpaka mtu aweze kuufikia ukweli yeye mwenyewe.

Socrates aliamini katika maisha ya misingi sahihi ya kifalsafa. Aliamini tuna kusudi kubwa la kuwa hapa duniani na siyo tu kuzaliwa, kuishi na kufa.
Kupitia kitabu hichi cha Socrates’ way, tutajifunza misingi saba ya kuiishi kwenye maisha yetu, ambayo itatuwezesha kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa.
Karibu kwenye safari hii ya #KURASA_KUMI kila siku, tujifunze kupitia maisha ya Socrates.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa