Katika uwekezaji kwenye hisa, kuna nyakati mbili ambazo wawekezaji huweza kutengeneza faida kubwa au kupata hasara kubwa. Nyakati hizi zimekuwa zikisoma uelekeo wa soko na watu kuchukua hatua ambazo zinawanufaisha au kuwapa hasara.
Nyakati hizo mbili ni kama ifuatavyo;
- Mbahatisha hisa (BEAR MARKET).
Hii ni hali inayotokea pale bei ya hisa inakuwa juu sana na mwekezaji mwenye hisa nyingi anapanga kuuza hisa zake zote, akitegemea bei itashuka na aweze kuninunua tena kwa bei ya chini. Kama mambo yataenda kama alivyopanga, basi atakuwa ametengeneza faida kubwa.
Kwa mfano kama hisa za kampuni A zimepanda bei kutoka 600 mpaka kufika labda 900 na mwekezaji kuona haziwezi kwenda zaidi ya hapo au kuna viashiria zitashuka bei, anaweza kuuza hisa zake, akitegemea zikishuka atanunua tena.
Kwa kuwa hisa zinakuwa juu, wengi hukimbilia kuzinunua na zinaposhuka wengi hukimbilia kuuza.

- Mlanguzi hisa (BULL MARKET).
Hii ni kinyume na kwenye mbahatisha hisa, ambapo hapa hisa zinakuwa na bei ndogo, mwekezaji anazinunua kwa wengi akiamini zitapanda bei na kuweza kuziuza kwa bei ya juu. Hapa hisa zinakuwa zimeshuka kiasi kwamba kinachofuata ni kupanda. Mwekezaji anaweza kuzinunua kwa bei hiyo ya chini ili zitakapopanda bei aziuze kwa bei juu.
SOMA; UWEKEZAJI LEO; Faida Tano Za Kuwekeza Kwenye Hatifungani.
Hali zote hizi mbili zinaendeshwa kwa hisia za watu, kwa sababu bei ya hisa inapopanda wengi hukimbilia kununua na pale inaposhuka wengi hukimbilia kuuza. Hivyo unahitaji kudhibiti hisia zako ili kuweza kutumia hali hizo mbili.
Hali zote hizi mbili ni hatari, kwa sababu mtu huwezi kujua kwa hakika hisa zitapanda lini au kushika lini. Ni utabiri usiokuwa na uhakika, hivyo mwekezaji yeyote anayefanya ubahatishaji au ulanguzi, anapaswa kufanya akijua anaweza kupoteza.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog