KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to tje utmost / Ronald Gross.
UKURASA 51 – 60

Socrates alisifika kwa kuwa mtu wa kuhoji.
Hakuwa mtu wa kukubali chochote anachoambiwa na kukipokea kama ndiyo kitu kamili.
Badala yake alihoji zaidi na zaidi kuhakikisha anaupata ukweli wenyewe.
Na hata kwenye kushauri watu, hakukimbilia kuwasikiliza na kuwaambia kipi cha kufanya.
Badala yake aliwahoji maswali mpaka wao kuona wenyewe kipi wanaweza kufanya.

Siri kuu ya Socrates kwenye kujua mengi na hata kuwasaidia wengi ilikuwa kwenye kuuliza maswali makuu.
Aliuliza maswali yanayolenga kujua msingi halisi wa kitu na siyo matokeo pekee.

Hivyo kama tunahitaji kujua vitu kwa undani, kama tunataka kuwashauri wengine vizuri basi tunapaswa kuuliza maswali makuu kwenye kila jambo tunalotaka kujua au kushauri wengine.
Ubora wa maswali unayojiuliza au kuuliza wengine ndiyo utaamua maarifa unayopata au kutoa kwa wengine.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa