KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 71 – 80.
Maswali tunayojiuliza na hata kuwauliza wengine, yanachangia sana kwenye mtazamo ambao mtu unakuwa nao.
Ukijiuliza maswali chanya unajenga mtazamo chanya, kadhalika maswali hasi yanajenga mtazamo hasi.
Kwa mfano badala ya kujiuliza kwa nini hupati kitu fulani, jiulize unawezaje kupata kitu hicho. Kubadilika huko kwa swali kunabadili kabisa mtazamo wako na kuathiri matokeo unayopata.
Hata kwa wale wanaokuzunguka, unapokutana na mtu ambaye mtazamo wake ni hasi na anaona mambo hayawezekani, muulize maswali chanya ambayo yatamfanya afikiri tofauti.
Kama mtu anasema hana lolote linalomhamasisha kwa sasa, muulize lipi lingeweza kumhamasisha. Hapo atafikiri tofauti na kuanza kuona vitu anavyoweza kufanya.
Kama ambavyo Socrates alipendelea kuhoji na kujihoji kwa kila jambo, tuhakikishe tunajihoji kwa maswali chanya ili tuweze kuona hatua za kuchukua na kuwa bora zaidi.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa