Why do I not seek some real good; one which I could feel, not one which I could display? – Lucius Annaeus Seneca

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIFANYE ILI KUONEKANA….
Kwenye kila jambo tunalofanya kwenye maisha yetu, kuna msukumo unaotupelekea kufanya.
Msukumo huu unaweza kutoka ndani yetu wenyewe, au ukatoka nje yetu.

Msukumo wa ndani ni pale unapofanya kwa sababu ndiyo umejipa wajibu wa kufanya. Unafanya kwa sababu unajisikia vizuri kufanya hivyo. Msukumo huu ndiyo unaowawezesha watu kuwa bora na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Msukumo wa nje ni pale mtu anapofanya kitu ili aonekane, anafanya ili watu wamwone na yeyey yupo au na yeye anaweza kufanya. Msukumo huu hauleti mafanikio kwa sababu mtu hafanyi kwa uhalisia, bali kwa kuigiza. Hivyo chochote wnachopata, hakiwezi kumridhisha, kwa sababu siyo halisi kwake.

Chochote tunachokwenda kufanya leo, hebu tujipe sekunde chache na kujiuliza je tunafanya kwa sababu tunataka kufanya au tunafanya ili tuonekane?
Kama jibu ni kuonekana, acha na fanya kilicho sahihi.
Muda tulionao ni mchache, tuutumie kufanya yaliyo sahihi kwetu na wanaotuzunguka.

Nakutakia siku bora sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha wako.
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa