KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA 131 – 140.

Tumejifunza kwamba Socrates alikuwa anakutana na watu kila siku jioni mjini Anthens ambapo walikuwa na mijadala mbalimbali. Hii ni mijadala ambayo aliwachochea watu kuhoji na kujihoji zaidi ili kuweza kujua ukweli, kwa uhuru kabisa bila ya kulazimishwa au kupotoshwa.

Tunayo fursa ya kufanya hivi kwenye zama hizi.
Kwa kuchagua watu ambao unaweza kujadiliana nao kwenye mambo mbalimbali. Watu ambao wako huru kujifunza na kuwa bora zaidi badala ya kushikilia misimamo waliyonayo.

Unaweza kutengeneza kikundi hichi kwa watu ambao mnaweza kuwa mnakutana moja kwa moja na kujadiliana.
Lakini pia kama hilo haliwezekani, mnaweza kutumia mtandao wa intaneti mkatengeneza kundi ambalo mtakuwa mnaendesha mijadala ya kuhoji kila ambacho mnachagua kujadili.
Mnajadili kwa uhuru na kuheshimiana mpaka wote mnafika hatua kwamba mnakubaliana kwa hoja zilizotolewa, na siyo tu kuamua kuacha mjadala na kila mtu kuondoka na msimamo wake.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa