KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross
UKURASA; 151 – 160.
Licha ya kwamba Socrates hakuwa na umiliki wa mali yoyote ile,
Licha ya kudhihakiwa na watu wengi,
Na licha ya kuhukumiwa kifo na kuchagua kufa,
Socrates alikuwa mtu mwenye furaha na aliyeridhika na maisha yake.
Hii ni kwa sababu alikuwa imara sana kiroho.
Alijua na kuishi kusudi la maisha yake na alijua jinsi ya kutatua changamoto za maisha yake.
Socrates aliweza kuwa imara kiroho kwa kuzingatia misingi hii minne muhimu;
1. Kujidhibiti mwenyewe (self-control)
Socrates hakuruhusu mwili wake umwendeshe, bali yeye ndiye aliyeendesha mwili wake.
2. Kuwa halisi (Authenticity).
Socrates aliishi maisha yake kwa uhalisia wake. Hakujaribu kujizuia wala kutaka kuiga maisha ya wengine.
3. Kujitambua (Self-discovery).
Socrates alifanya kazi kuweza kujitambua yeye mwenyewe.
4. Kujiendeleza (Self-development)
Socrates alikuwa tayari kujifunza na kupiga hatua kila siku ya maisha yake.
Tuzingatie mambo haya manne na tutaweza kujijenga na kuwa imara kiroho.
Kocha Makirita Amani.
http://www.amkamtanzania.com/kurasa