KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 161 – 170.

Kama ilivyokuwa kwa Socrates, kila mmoja wetu ana kitu ndani yake, ambacho kinaweza kuinufaisha dunia.
Kitu hichi kinatoka ndani yake na kwakukifanya mtu anapata furaha na kuridhika sana.
Na hata kama mtu halipwi, atakuwa tayari kufanya kitu hicho.

Socrates na hata wanasaikolojia wa sasa wanatuambia kitu hichi ni muhimu sana katika kuimarisha roho zetu.
Unapopata nafasi ya kufaya kile unahopenda, ukiona mchango unaotoa kwa wengine, unaridhika sana.

Kwa Socrates kitu hichi kilikuwa kufundisha na kuhoji watu ili waone kama wapo sahihi kweye kile wanachosimamia. Aliendelea kufanya hilo mpaka siku anakufa.

Wewe pia una kitu ndani yako, ambacho kinaweza kuwanufaisha wengine. Kijue na anza kufayia kazi ili wengine wanaufaike.
Inawezekana kilichopo ndani yako ni uandishi, unenaji, ufundishaji, ushauri n.k.
Jua hasa kile kilichopo ndai yako, na kila siku kifanyie kazi ili kuwa bora zaidi.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa