Wherever there is a human being, there is an opportunity for a kindness. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera rafiki yangu kwa siki hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FURSA YA KUWA MWEMA…
Jukumu letu kubwa kama wanadamu, ni kuwa watu wema.
Tunahitaji kuwa wema kwetu binafsi, kwa wale wanaotuzunguka na hata mazingira yetu.
Bila ya wema, dunia itakuwa sehemu hatari sana ya kuishi.

Watu wengi hujiuliza ni mahali gani na wakati gani wa kuwa mwema.
Na jibu ni kila wakati, kila palipo na mtu ni fursa nzuri ya kuwa mtu mwema.
Chochote unachofanya kwenye maisha yako, fanya kwa kusudi la kutoa thamani zaidi kwa wengine. Fanya kwa kutoa kitu kitakachoboresha zaidi maisha ya wengine.
Huo ndiyo unaitwa utu, huo ndiyo ubinadamu. Kama hufanyi hivi, hustahili kuwa binadamu.

Nenda kawe mwema leo, kwa kila unachofanya.
Nakutakia siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa