Dunia inapenda matokeo, ila haipendi mchakato. Watu wanafurahia na kuhamasika pale wanapoona mtu kapata matokeo fulani mazuri na makubwa. Lakini hawapendi kuona mchakato mzima uliozalisha matokeo yale, na hata wakiambiwa mchakato huo, wanaweza wasikubaliane nao.

Tunapoishi maisha yetu, tunapanga michakato ambayo inatufikisha kwenye mafanikio. Watu wengi huzama kwenye mchakato, kwenye kila hatua wanayopiga kiasi cha kuchoshwa na hatua hizo na kushindwa kupata matokeo wanayoyataka.

siyo ajali

Sasa leo nataka tuangalie matokeo na mchakato, na wakati sahihi kwa kila kimoja.

Wakati dunia inashangilia matokeo, wewe kazana kuangalia mchakato. Wakati watu wanapata hamasa kutokana na matokeo yanayoonekana kwa nje, wewe tafuta kujua mchakato ambao huwa hata hauonekani. Kwa njia hiyo utajua nini unapaswa kufanya ili kufika kwenye matokeo yale.

Unapokuwa unafanya wewe, ukishajua matokeo unayotaka kufikia, usipoteze muda kwenye mchakato. Badala yake tengeneza mfumo, ambao unakupeleka kwenye yale matokeo unayotaka. Tengeneza mfumo ambao utabeba kila mchakato, ambapo wewe utakuwa tu na hatua za kuchukua kila siku na kila wakati, huku ukiangalia matokeo makubwa unayotaka kuyafikia.

SOMA, #TAFAKARI YA LEO; USISUBIRI KUAMBIWA….

Kwa kuangalia matokeo, utaweza kutengeneza njia mbadala pale unapokutana na changamoto kwenye njia uliyochagua. Kwa kuwa unajua wapi unataka kufika, ni rahisi kuona njia nyingine za kufika pale.

Unapokazana na mchakato pekee, anapoangalia yale unayofanya pekee, ni rahisi kukata tamaa na kuona haiwezekani tena pale unapokutana na vikwazo au changamoto.

Matokeo na mchakato vyote ni muhimu, kama ukijua wapi unapaswa kutumia kipi. Usiwe kama wengi ambao wanashangilia matokeo na wasijue mchakato, au wanaokazana na mchakato na wasione matokeo makubwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog