If you want to improve, be content to be thought foolish and stupid. – Epictetus
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa nafasi hii ya kipekee sana ya leo.
Nafasi ambayo wapo ambao wangelipa mamilioni ya fedha ili waione na waitumie, lakini hawajapata nafasi hii.
Lakini wewe umeipata, swali ni je unaitumiaje?
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUBALI KUONEKAMA MJINGA….
Kama kipo kitu ambacho kila mtu anakikimbia, basi ni kuonekana mjinga.
Kila mtu anapenda kuonekana anajua, hata kama hajui.
Watu hawapendi kabisa kusema neno SIJUI, au nisaidie, au nifundishe.
Wengi hawajui, lakini wanajifanya wanajua.
Huwezi kupiga hatua kwenye maisha kama tayari unajua kila kitu.
Ukishajiona unajua kila kitu, jua imechagua kufika ukomo wa maisha yako. Hutajifunza tena wala kupiga hatua.
Utaendelea kuwa na maisha magumu wakati wenzako wanapiga hatua.
Kubali kuonekana mjinga, lakini ujifunze.
Sema hujui na kubali kufundishwa.
Kila mtu, nirudie KILA MTU, ana kitu cha kukufundisha.
Kuwa tayari kufundishika na utafaidi mengi.
Uwe na siku bora sana ya leo rafiki.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa