KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA 67 – 76.

Moja ya misingi ambayo ilimwezesha Leonardo kufanya makubwa ni kuwa tayari kujifunza kupitia uzoefu anbao alikuwa anapitia.
Leonardo aliishi kipindi ambacho watu walikuwa wanaamini hakuna elimu mpya, kila kitu kimeshajulikana.
Hivyo hakuna aliyehoji wala kujifunza zaidi.

Leonardo hakukubaliana na hilo,
Alikuwa tayari kujifunza kupitia kile ambacho alikuwa anakutana nacho kila siku.
Alihoji zaidi na kila alichoona alikichukua kwa uzito wa hali ya juu.

Leonardo pia alikuwa tayari kukosea, na licha ya kujulikana kwa kazi nyingi na kubwa, yapo mambo mengi aliyojaribu lakini akashindwa.
Kwa mfano alikuwa na mipango ya kutengeneza kitu cha kumwezesha mtu kupaa kama ndege, lakini hakuweza kufanikiwa.

Kama kweli tunataka kupiga hatua kwenye maisha yetu, lazima tuwe tayari kujifunza vitu vipya, na lazima tuwe tayari kukosea.
Unapokosea unajifunza zaidi kupitia makosa yako.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa